NDC KULETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA VIFAA TIBA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Innocent Bashungwa amelitaka Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kuharakisha mchakato wake wa kuanzisha kiwanda cha kuzalisha vifaa tiba kama barakoa na gloves, kinachotarajiwa kujengwa katika Eneo la Viwanda la TAMCO, Kibaha mkoani Pwani. Ameyasema hayo mapema leo jijini Dar es Salaam wakati wa Kikao cha Wadau kujadili upatikanaji […]

NDC KUZALISHA VIFAA TIBA

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) lipo mbioni kuanzisha kiwanda cha kuzalisha vifaa tiba (barakoa, gloves pamoja na vifaa tiba vingine) katika eneo la viwanda TAMCO, mkoani Kibaha,  ikiwa ni jitihada za Shirika katika kupambana na ugonjwa wa Corona pamoja na kuendeleza sera ya Tanzania ya Viwanda. Hayo yamesemwa mapema leo na Kaimu Mkurugenzi wa […]

NDC yadhamiria kuinua viwanda nchini

NDC kwa kushirikiana na TANCOAL wamemkabidhi Mzee Reuben Mtitu (Mzee Kisangani) tani 60 za makaa ya mawe kwa ajili ya kuendeleza kazi yake ya uhunzi, Ludewa mkoani Njombe. Mzee Mtitu alianza shughuli ya uhunzi miaka 20 iliyopita na anaishukuru Serikali, NDC pamoja na TANCOAL kwa msaada huo kwani utatimiza azima yake ya kuendeleza Tanzania ya […]

Jarida la Maendeleo

Pakua Jarida la Maendeleo http://ndc.go.tz/wp-content/uploads/2020/03/Jarida-la-Maendeleo-NDC.pdf

Kamati ya Bunge yatembelea TAMCO

Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imetembelea eneo la viwanda la TAMCO lililopo Kibaha, mkoani Pwani. Katika ziara hiyo wametembelea na kujionea viwanda mbalimbali vilivyopo katika hatua ya ujenzi kama kiwanda cha GF Trucks kinachotarajiwa kuunganisha magari pamoja na kiwanda cha kuzalisha chanjo za wanyama cha Heister Bioscience Africa Ltd. Mbali na hapo, […]

Bashungwa atembelea TAMCO

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amefanya ziara ya kikazi kwenye eneo la Viwanda la TAMCO lililopo Kibaha mkoani Pwani. Katika ziara hiyo ametembelea kiwanda cha kuunganisha matrekta cha Ursus, kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging pamoja na kiwanda cha kuzalisha chanjo za wanyama cha Heister Bioscience Africa ltd. Amefurahishwa na hatua mbalimbali […]

Bashungwa atembelea TBPL atoa maagizo

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amekiagiza kiwanda cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) kuhakikisha kina tokomeza malaria kwa kuongeza kasi ya kutafuta masoko ya viuadudu. Ameyasema hayo mapema leo alipo tembelea kiwanda hicho Kibaha, mkoani Pwani katika ziara ya kikazi. Amesema kuwa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kupitia kiwanda chake cha TBPL […]

ZABUNI YA KUUZA VIUADUDU

SHIRIKA LA TAIFA LA MAENDELEO MWALIKO WA KUONESHA NIA YA KUWA WAKALA WA UUZAJI WA VIUADUDU VINAVYOZALISHWA NA KAMPUNI YA TANZANIA BIOTECH PRODUCT LIMITED UTANGULIZI Tanzania Biotech Product Limited (TBPL) ni kampuni tanzu ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) inayozalisha viuadudu katika kiwanda chake kilichopo Kibaha, Mkoa wa Pwani. Viuadudu ni bidhaa za kibiolojia […]

NDC YATOA GAWIO KWA SERIKALI

Tunapenda kuitaarifu Watanzania wote kuwa, katika kutimiza wajibu kwa Taifa, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limewasilisha kwa Serikali, gawio la Shilingi 185, 950,000/=. Gawio hili liliwasilishwa rasmi kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma mnamo tarehe 8 Januari 2020. Gawio hilo liliwasilishwa na Mkurugenzi Mwendeshaji […]

MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA 5 KUPITIA SHIRIKA LA TAIFA LA MAENDELEO (NDC)

Katika kuhakikisha Tanzania inafikia adhma ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) linajivunia mchango wake katika ujenzi wa taifa kwa kipindi cha miezi 18 kutoka April 2018 hadi Disemba 2019. Kwa kuzingatia juhudi, na nia ya dhati ya Mheshimiwa Rais wetu kipenzi, Dr. John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi […]