UJUMBE WA SADC WATEMBELEA TBPL

Ujumbe maalum kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umetembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi wa mbu waenezao Malaria, Tanzania Biotech Product Limited (TBPL) kilichopo Kibaha mkoani Pwani. Ziara ya kutembelea kiwanda imefanyika katika kilele cha Wiki ya Viwanda ya SADC iliyofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 9, Agosti 2019 […]

NAIBU WAZIRI VIWANDA AHAMASISHA WAKULIMA KUCHANGAMKIA MATREKTA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Eng. Stellah Manyanya ametembelea banda la Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwenye Maonesho ya wakulima Nanenane, mkoani Simiyu kwenye viwanja vya Nyakabindi. Amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kununua viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu vinavyo zalishwa na TBPL pamoja na matrekta ya Ursus yanayo unganishwa na NDC ili […]

NDC yashiriki Maonesho ya Wakulima (NANENANE)

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limeshiriki kwenye Maonesho ya 27 ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika mkoani Simiyu kwenye viwanja vya Nyakabindi. Katika maonesho hayo yaliyofunguliwa tarehe 1 na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limejizatiti kuonesha miradi miwili ya kimkakati inayolenga kuwainua Watanzania […]

Tanzania tayari kuelekea wiki ya SADC

Kuelekea wiki ya Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kuanzia tarehe 5 hadi 9 mwezi wa 8, 2019. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Innocent Bashungwa amewataka wamiliki na wadau wa sekta ya viwanda kujitokeza kwa wingi. Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Taifa […]

NDC yazindua tela la mizigo

Kwa kuwajali wakulima na watumiaji wa matrekta ya Ursus yanayouzwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Innocent Bashungwa amezindua tela la kubebea mizigo lenye uwezo wa kubeba mzigo wa tani mbili hadi 2.5 Hafla hiyo imefanyika kwenye viwanja vya kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC), Kilimanjaro. Amezipongeza […]

Waziri wa Viwanda atembelea KMTC

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Innocent Bashungwa akiongozana Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lenga Ole Sabaya, Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC, Prof. Damian Gabagambi wametembelea kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC) kilichopo mkoani Kilimanjaro. Akiwa kiwandani hapo, amejionea shughuli mbalimbali zinazo fanyika katika kuinua Tanzania ya viwanda. […]

NDC kuinua kilimo Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mh. Aggrey Mwanri kwa kushirikiana na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) amekabidhi matrekta 14 kwa vyama vya ushirika vya mkoa huo (Igembesabo) katika hafla iliyofanyika wilayani Igunga mkoani Tabora. Mbali na vyama vya ushirika, Mkuu wa Mkoa amekabidhi matrekta kwa watu binafsi wakiwemo Mapadri, Maaskofu na Masheikh wa mkoa […]

Ndugai aula treka la Ursus

Azma ya kupeleka jembe la mkono makumbusho inazidi kupiga kasi baada ya Spika wa Bunge la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kukabidhiwa trekta na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) mkoani Dodoma. Katika hafla iliyofanyika Mbande, Dodoma, Spika Job Ndugai amelipongeza Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa mradi wao wa matrekta kwani […]

TBPL YAPATA BODI MPYA

Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayopambana kuhakikisha yanautokomeza kabisa ugonjwa wa malaria. katika kuunga mkono jitihada hizo, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limezindua bodi mpya ya wakurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha viuadudu viangamizavyo viluwiluwi vya mbu (TBPL). Kiwanda hicho ni ushirikiano wa serikali ya Tanzania na Cuba ni muhimu katika mapambano dhidi ya malaria […]

NDC kuleta mapinduzi sekta ya kilimo