Bashungwa atembelea TAMCO

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa akiteta jambo na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Prof. Damian Gabagambi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amefanya ziara ya kikazi kwenye eneo la Viwanda la TAMCO lililopo Kibaha mkoani Pwani.

Katika ziara hiyo ametembelea kiwanda cha kuunganisha matrekta cha Ursus, kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging pamoja na kiwanda cha kuzalisha chanjo za wanyama cha Heister Bioscience Africa ltd.

Amefurahishwa na hatua mbalimbali zinazofanywa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) katika kuendeleza Tanzania ya viwanda na kuwasihi wanapopata changamoto yoyote wasisite kumuona ili watatue changamoto hizo kwa maendeleo mapana ya taifa.

Eneo la viwanda la TAMCO lina ukubwa wa hekari 201.63 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya sekta mbalimbali kama dawa, kilimo, nguo na vyombo vya moto.