MAJALIWA ataka, Halmashauri, Wananchi kutumia Viuadudu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awataka halmashauri zote, taasisi na watu binafsi kununua na kutumia dawa za viuadudu ili kutokomeza malaria nchini wakati alipotembelea kiwanda cha TBPL kinachozalisha viuadudu katika eneo la Tamco Kibaha Pwani siku ya jumatano 29.08.2018.
‘Nimekuta lundo la dawa za viuadudu hazijapata soko ‘ alisema Waziri Mkuu.
Mwaka jana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuri aliagiza halmashauri zote nchini kununua na kutumia viuadudu.

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa utumiaji wa Viuadudu yapaswa kuwa endelevu na juhudi za msingi zaidi katika kutokomeza malaria kabda ya jitihada zingine.

Teknolojia hii ya Viuadudu imejikita katika kuua viluilui wa mbu hivyo kuzuia kuzaliana kwa mbu.

Nimeambiwa kuwa dawa hizi pia zinaweza kutumika majumbani na watu binafsi hata taasisi aliongeza Majaliwa.

Mbu wanazaliana hasa kwenye maeneo ya maji yaliyotuama kama visima, madimbwi, mashimo ya vyoo na hata kwenye vyombo vya kuhifadhia maji.

Pia Mkuu wa mkoa Pwani Mwandisi Everist Ndikilo aliwatoa hofu wananchi kuwa dawa hiyo haina madhara kwa afya ya binadamu kwani wafanyakazi wa kiwanda walishawahi kuinywa dawa mbele yake katika kumdhibitishia usalama wa Viuadudu kwa viumbe hai.
*****************
Katika hatua nyingine

‘Nimefarijika pia kukuta watanzania wakinipa maelezo ya hatua zote za uzalishaji wa viuadudu. Maana yake ni kwamba sasa tumemudu teknolojia hii toka Cuba’
Pia Wazari Mkuu alionyesha matumaini na maandalizi ya wataalamu wazawa katika kukiongoza kiwanda hicho siku za usoni.
Nina matumaini wakati wowote wataalamu wa Cuba wakiondoka na kutuachia kiwanda kutakuwa na wataalamu watanzania wenye uwezo wa kukiendesha kiwanda, alisema Majaliwa.

Ikumbuke kuwa kiwanda cha TBPL ni cha pekee barani Afrika ambacho kwa sasa kinatengeneza Viuadudu wa kuangamiza viluilui wa mbu.