Matrekta yanayouzwa nchini na NDC sasa kupatikana Mwanza

Tunawakaribia wateja
NDC yapeleka Mwanza matrekta 27 na zana zake ili kurahisisha soko na usafirishaji kwa wateja wake wa kanda ya ziwa.
Huu ni utekelezaji wa awali katika kuwakaribia wateja kwa kuanzisha vituo vya Kikanda vya kuuza, kufundisha madereva na kutoa huduma za baada ya mauzo kwa matrekta hayo na wateja.
“Mpango wetu ni kupeleka matrekta mengi zaidi nchi nzima ila kwa kuanzia tutapeleka matrekta 50 Mwanza” amesema Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC Prof Damian Gabagambi