NAIBU WAZIRI VIWANDA AHAMASISHA WAKULIMA KUCHANGAMKIA MATREKTA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Eng. Stellah Manyanya akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la NDC kwenye maonesho ya Nanenane mkoani Simiyu, 2019

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Eng. Stellah Manyanya ametembelea banda la Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwenye Maonesho ya wakulima Nanenane, mkoani Simiyu kwenye viwanja vya Nyakabindi.

Amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kununua viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu vinavyo zalishwa na TBPL pamoja na matrekta ya Ursus yanayo unganishwa na NDC ili waweze kuboresha afya zao na kujikwamua kiuchumi.