NDC kuleta mapinduzi sekta ya kilimo

Ili kuleta mapinduzi ya viwanda na kuinua sekta ya kilimo nchini, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa kupitia mradi wa matrekta ya Ursus wamedhamiria kusambaz matrekta nchi nzima.

Akifafanua hilo katika hafla ya kukabidhi matrekta 7 kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) iliyofanyika Tamco, Kibaha mkoani Pwani, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Prof. Damian Gabagambi alisema kuwa mpaka sasa wamesha sambaza jumla ya matrekta takriban 300.

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) likiwa limesambaza matrekta 348 kwa kushirikiana na taasisi nyingine pamoja na wanunuzi binafsi.
.
“Wakati unakuja hapa tulikuomba utupe kibali cha kuyauza, ukaturuhusu na sasa yameenda shambani,” alisema Prof. Gabagambi.

Aliongeza kuwa lengo la serikali sio kufanya biashara ili kupata faida katika mradi wa matrekta bali faida pekee ni kuona kilimo kilicho badilika.

“Tunataka tuhakikishe matrekta yanapatikana kwa wakulima wote nchi hii,” alisema Prof. Gabagambi.

Alitaja mikoa inayo ongoza kwa kuwa na matrekta mengi ni Manyara ikiwa na matrekta 136, Morogoro 67, Mwanza 37, Ruvuma 40 na Arusha 28.

“Pia kuna taasisi ambazo zimeshachukua matrekta ikiwemo Magereza, SUA na leo TALIRI imeongezeka,” alisema Prof. Gabagambi.

Amewaomba wanaochukua matrekta kuyatunza kwani ndio chanzo cha mafanikio.
“Hatuhitaji riba, mkulima anatanguliza kiasi fulani na anapewa trekta,” alisema Prof. Gabagambi.

Ili kuweza kurejesha kwa haraka mkopo wa matrekta aliwasihi wanaochukua matrekta kuyatumia katika shughuli mbalimbali kama kusomba maji, kuni, kulima, kipanda, kumwagilia, kuzalisha umeme.

“Hiki ni kiwanda,” alisema Prof. Gabagambi.

Tulianza kutoa trekta, plau na halo, kwa kuwajali wateja wetu tumeamua kuwaongezea bidhaa mpya kwani tumeona wanahitaji zaidi ya hayo.

“Tumeshatengeneza tela, bado kuzisambaza,” alisema Prof. Gabagambi.

Kwa kuwajali wakulima, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kupitia mradi wake wa matrekta ya Ursus umejipanga kuongeza bidhaa nyingine kama kisomba nyasi (bellar) kwa ajili ya wakulima wa nyasi, mashine za kupanda (planter), mashine za kupulizia dawa (boom sprayer) na mashine nyingine.

“Tuziombe taasisi ntingine za kilimo na ufugaji zije tuwape matrekta,” alisema Prof. Gabagambi.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC aliwapongeza wafanyakazi wa shirika lake kwa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha yote haya yanawezekana.