NDC KUPUNGUZA MATUMIZI YA KARATASI

Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) wakisikiliza mafunzo juu ya Tehama katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi.

Katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, hatuna budi kupunguza matumizi ya karatasi ili kulinda miti na uoto wa asili.

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limejidhatiti kupunguza matumizi ya karatasi katika shughuli zake za kila siku kwa kujikita katika kubadilisha mifumo ya uendeshaji wa shughuli zake kwa kutumia teknolojia yenye manufaa.

Mkakati huo unaenda sambamba na mafunzo juu ya teknolojia ya kisasa ambapo wafanyakazi wa NDC (hawapo pichani) wamepata fursa ya kujifunza matumizi ya teknolojia hiyo kutoka kwa wakufunzi Luis William, Mtaalam wa Tehama na Catherine Christian, Afisa Mahusiano kwa Wateja kutoka NPK TECHNOLOGY LIMITED.

Inaelezwa kuwa matumizi sahihi ya teknolojia yataongeza ufanisi wa kazi na kupunguza mlolongo wa maamuzi, usiri katika kazi na kuokoa muda katika shughuli za kila siku.