NDC wawafurahisha Magufuli, Museveni

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wamefurahishwa na kazi nzuri inayofanya na Edosama Hardware Limited kwa kutengeneza samani kwa kutumia mbao mbadala (MDF BOARD) katika Kongamano la Kwanza la Biashara baina ya Tanzania na Uganda katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Rais Magufuli amefurahishwa na kazi nzuri waliyoifanya Edosama Hardware Limited kwa kutumia magogo ya miti aliyowakabidhi Ikulu kutengeneza kibweta chenye ramani ya Afrika na kuwahaidi kuwapa magogo mengine yaliyopo Ikulu watengeneze samani.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kuvutiwa na kibweta hicho chenye ramani ya Afrika, amewaomba Edosama Hardware Limited kutengeneza ramani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Mradi wa MDF Board ni ubia baina ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na Edosama Hardware Limited.