NDC YATOA GAWIO KWA SERIKALI

Tunapenda kuitaarifu Watanzania wote kuwa, katika kutimiza wajibu kwa Taifa, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limewasilisha kwa Serikali, gawio la Shilingi 185, 950,000/=.

Gawio hili liliwasilishwa rasmi kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla iliyofanyika jijini Dodoma mnamo tarehe 8 Januari 2020.

Gawio hilo liliwasilishwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Prof. Damian Gabagambi.

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) linaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuboresha maisha ya Watanzania na kupunguza utegemezi kutoka mataifa mengine.