NDC yazindua tela la mizigo

Kwa kuwajali wakulima na watumiaji wa matrekta ya Ursus yanayouzwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Innocent Bashungwa amezindua tela la kubebea mizigo lenye uwezo wa kubeba mzigo wa tani mbili hadi 2.5

Hafla hiyo imefanyika kwenye viwanja vya kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC), Kilimanjaro.

Amezipongeza taasisi zilizo chini yake, NDC, CAMARTEC, KMTC pamoja TEMDO kwa kusanifu na kuunda tela hilo.

“Tela hili litakuwa la manufaa kwa wakulima baada ya kuvuna,” alieleza Bashungwa.

Katika hatua nyingine, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) linatarajia kuzindua tela jingine lenye uwezo wa kubeba mzigo wa tani 5 ifikapo mwezi wa 8 mwishoni.