Tanzania tayari kuelekea wiki ya SADC

Kuelekea wiki ya Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kuanzia tarehe 5 hadi 9 mwezi wa 8, 2019. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Innocent Bashungwa amewataka wamiliki na wadau wa sekta ya viwanda kujitokeza kwa wingi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Waziri amesema lengo la wizara yake ni kuvutia wawekezaji.

Pia amesisitiza kuwa shabaha yao ni kuongeza mahuruji (export) kuliko maduhuli (import).

Ikumbukwe kuwa Tanzania ndiye mwenyeji wa mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo pamoja na mambo mengine, Tanzania imelenga kutumia wiki hiyo kuonesha maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya viwanda.