TBPL YAPATA BODI MPYA

Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayopambana kuhakikisha yanautokomeza kabisa ugonjwa wa malaria.

katika kuunga mkono jitihada hizo, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limezindua bodi mpya ya wakurugenzi wa Kiwanda cha kuzalisha viuadudu viangamizavyo viluwiluwi vya mbu (TBPL).

Kiwanda hicho ni ushirikiano wa serikali ya Tanzania na Cuba ni muhimu katika mapambano dhidi ya malaria na dengue.

“Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, (SADC) wameonesha uhutaji wa dawa,” alisema Dkt. Samuel Nyantahe, Mwenyekiti wa Bodi ya NDC.

Aliongeza kuwa, kiwanda ni muhimu sana katika kutokomeza malaria hivyo ni muhimu watu wakafahamu matumizi sahihi ya dawa hizo.

Dkt. Samuel Nyantahe, aliipongeza Wizara ya Afya kwa kuchukua dawa nyingi zaidi.

Pia aliishauri bodi mpya kuja na mikakati ya kibunifu ili kuleta ushindani katika soko.

Kiwanda cha kuzalisha viuadudu viangamizavyo viluwiluwi vya mbu (TBPL) kilichopo Kibaha, Pwani kilifunguliwa rasmi na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Julai 2, 2015.