TUMEDHAMIRIA KUWA BORA KATIKA HUDUMA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejidhatiti kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Ili kufikia malengo hayo, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wameamua kutoa mafunzo juu ya viwango na ubora, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa NDC.

Mafunzo hayo yanayofahamika kama ISO 9001:2015 yameendeshwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Jumatano hadi Ijumaa kwa wafanyakazi wa NDC.

Ikumbukwe kuwa NDC ina jukumu la kuwa mkono wa uwekezaji wa Serikali, hivyo mafunzo ya ubora yatawaongezea wafanyakazi ufanisi katika shughuli zao za kila siku za kujenga taifa na kuchochea ari ya maendeleo nchini.