UJUMBE WA SADC WATEMBELEA TBPL

Ujumbe maalum kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umetembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi wa mbu waenezao Malaria, Tanzania Biotech Product Limited (TBPL) kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Ziara ya kutembelea kiwanda imefanyika katika kilele cha Wiki ya Viwanda ya SADC iliyofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 9, Agosti 2019 jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, ujumbe huo maalum ulipata fursa ya kutembelea eneo la kiwanda na kujifunza jinsi ya kuangamiza mazalia ya mbu.

Pia walipata wasaa wa kujionea uzalishaji wa viuadudu aina ya Bactivec na Griselesf ambavyo ni mahususi kwa kuangamiza viluwiluwi wa mbu waenezao ugonjwa wa Malaria, Dengue, Matende na Mabusha pamoja na magonjwa mengine yaenezwayo na mbu.

Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi wa mbu waenezao Malaria, Tanzania Biotech Product Limited (TBPL) kilichopo Kibaha mkoani Pwani kinamilikiwa kwa 100% na Serikali ya Tanzania chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).