Waziri wa Viwanda atembelea KMTC

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Innocent Bashungwa akiongozana Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lenga Ole Sabaya, Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC, Prof. Damian Gabagambi wametembelea kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC) kilichopo mkoani Kilimanjaro.

Akiwa kiwandani hapo, amejionea shughuli mbalimbali zinazo fanyika katika kuinua Tanzania ya viwanda.

Pia ameuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanajikita katika kuwainua Watanzania kiuchumi kupitia zana za kilimo na kuwataka wazidishe uzalishaji zaidi na kujitangaza.

Aliongeza kuwa inawapasa wafungue maduka ya kuuza vipuri vinavyo zalishwa kiwandani hapo katika maeneo mbalimbali ya nchi ili watumiaji wavipate kiurahisi.

Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC) kipo chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)