Wizara ya Viwanda na NDC kushirikiana kutatua Changamoto za Miradi

Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji imekutana na baadhi ya taasisi zilizopo chini yake ikiwemo NDC na EPZA ili kujadili mambo mbalimbali ya kiutendaji katika kutimiza majukumu na kushirikishana ujuzi ili kufikia lengo la serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda.
Aidha kikao kilipitia maelekezo ya Baraza la Mawaziri na kujadili uendelezaji wa miradi malimbali ikiwa ni pamoja na; eneo la viwanda la TAMCO lililopo Kibaha Pwani na mradi wa Mchuchuma na Liganga.
Katika kikao hicho kilichofanyika jana tarehe 17.09.2018 katika ukumbi wa mikutano wa NDC, Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mh Charles Mwijage, aliambatana na Naibu waziri Mh Stella Manyanya, Katibu Mkuu wa wizara Prof Joseph Buchweshaija na Naibu Katibu Mkuu Ludovick Nduhiye, pamoja nao, Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC Prof Damian Gabagambi na mangementi ya NDC, na Mkurugenzi Mkuu wa EPZA mstahafu Col.Joseph Simbakalia na managementi ya EPZA.