ABOUT US

The National Development Corporation (NDC) is a leading industrial development.

The National Development Corporation (NDC) is a leading industrial development and promotion organization established in 1962 as Tanganyika Development Corporations (TDC) by an Act of Parliament to fill the gap of financing critical development projects and take over the colonial development corporation (CDC) formed in 1950. In 1965, NDC was re established by the government to catalyze economic development in all sectors of the economy...

NEWS AND UPDATES

NDC na mchango katika Tanzania ya Uchumi wa Kati

Mnamo Julai Mosi 2020, Benki ya Dunia ilichapisha ripoti iliyo onesha kuwa Tanzania imeingia  katika nchi ya Uchumi wa Kipato cha Kati, hiyo ilikuwa ni hatua kubwa kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli na kwa taifa kwani ilivuka malengo iliyojiwekea ya kufika Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025.Miongoni mwa sababu zilizopelekea Tanzania kuingia katika nchi ya Uchumi wa Kipato cha Kati inatajwa kuwa ni utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati iliyobuni ajira kwa Watanzania wengi.kwa mujibu wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, (2025) ukurasa wa 2, kipengele (1.2) inasema ”Uchumi wa kipato cha kati umehusishwa na kuwa na nchi ambayo umaskini unapungua, uchumi imara unaojengwa na kuimarika kwa uzalishaji viwandani unaimarika na wananchi wanapata maendeleo.”Ili kuhakikisha taifa linaendelea kukuza uchumi wake na kufikia malengo makubwa zaidi, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limeona ni busara kuwanoa wafanyakazi wake katika Nyanja ya Uwekezaji hasa katika sheria ya Uanzishwaji na Usimamizi wa Miradi kwa Njia ya Ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership) ili kuendana na kasi ya Serikali katika kuhimiza uwekezaji na ukuaji wa pato la taifa na la mtu mmoja mmoja kwani NDC ni miongoni mwa taasisi zinazo tekeleza miradi ya kimkakati inayobuni ajira kwa watanzania wengi wa vipato tofauti tofauti.Kwa siku mbili mfululizo kuanzia tarehe 22.07.2020 hadi 23.07.2020, wakufunzi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakiongiozwa na Dr. John Mboya wameendesha Semina Elekezi kwa baadhi ya wafanyakazi wa NDC wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika, Prof. Damian Gabagambi, ili kuwajengea uwezo utakaowasaidia kulinufaisha taifa kupitia rasilimali zake.Semina hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa NDC, jijini Dar es Salaam ilihusu Masuala ya Uanzishwaji na Usimamizi wa Miradi kwa Njia ya Ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership) na ilijikita hasa katika Sheria ya Ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership Act) ya  mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017. NDC ikiwa ni mkono wa Serikali katika uwekezaji, ina miradi kadha wa kadha katika sekta mbalimbali kama; kilimo, Afya, Madini, na Nishati, hivyo mafunzo haya yalilenga kuwawezesha wafanyakazi kuelewa sheria na miongozo ya ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi. Kulingana na kifungu cha 4 (5) cha Sheria ya Uanzishwaji na Usimamizi wa Miradi kwa Njia ya Ubia baina ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership) ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho 2017 ina ainisha sekta kadha wa kadha zinazo angukia katika Ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi kama; Kilimo, Miundombinu, Viwanda, Madini, Afya, elimu, Mazingira, Biashara na Uwekezaji, hivyo Shirika halikuwa na budi kuwawezesha wafanyakazi wake kuelewa namna ya kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji kwa kuvutia uwekezaji, kukabiliana na changamoto mbalimbali na jinsi ya kuzitatua ili kusaidia taifa kunufaika na rasilimali zake.Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ni taasisi inayo chochea na kuongoza Maendeleo ya Viwanda iliyoanzishwa mwaka 1962, ikijulikana kama Shirika la Maendeleo Tanganyika (TDC) kwa Sheria ya Bunge ili kufadhili miradi muhimu ya kimaendeleo na kuchukua nafasi ya Shirika la Kikoloni la Maendeleo (CDC) lililo anzishwa mwaka 1947/1948.               

KEY PROJECTS

The Corporation intends to establish large scale commercial farming of Oil Palm and refinery plant in Kigoma Region in partnership with strategic private investment partner. This follows a feasibility study conducted for establishment of the project in the Coast Region.

 • AGRO INDUSTRIES

  Intergrated Oil Palm and Edible Oil Production Project. The Corporation intends to establish large


 • BIOLOGICAL INDUSTRIES

  The Biolarvicides Project - Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) is a subsidiary company of National Development


 • CHEMICAL INDUSTRIES

  Engaruka Basin Soda Ash Project - The project is located at Engaruka Basin, Monduli District, Arusha Region about 160 km


 • IRON AND STEEL METALLURGICAL COMPLEX

  Liganga Iron and Steel project - The project is located at Liganga area, Ludewa District, Njombe Region about 850


 • POWER PRODUCTION

  Mchuchuma Coal to electricity Project - The project is located at Mchuchuma area, Ludewa District, Njombe Region about 950 km


NDC tumedhamiria kuijenga Tanzania ya viwanda