Farm Implements

Engaruka Basin Soda Ash Project

Katika kuuza matrekta ya aina ya URSUS na zana zake, Shirika linatumia mifumo miwili yaani mfumo wa fedha taslim na mfumo wa mkopo.

1. Mauzo kwa Fedha Taslimu

Mteja atahitaji kulipia kwenye akaunti ya Shirika baada ya kuwasilisha mahitaji yake rasmi na kupewa Invoice ya NDC. Mteja atatakiwa kukabidhi kumbukumbu zake NDC kwa ajili ya usajili wa trekta. Kama sehemu ya huduma kwa mteja, Shirika litamkabidhi mteja trekta likiwa limeshasajiliwa. Mteja anaweza kuwasiliana na nasi kwa anuani ifuatayo:

Mkurugenzi Mwendeshaji, Shirika la Taifa la Maendeleo, Jengo la Development House, Mtaa wa Kivukoni Front/Ohio S. L. P. 2669, DAR ES SALAAM Simu: +255 22 2112893, 2111494, 2111460 Barua Pepe: md@ndc.go.tz

2. Mauzo kwa Mikopo Kupitia Taasisi za Fedha

i.) Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB)

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)limeingia mkataba na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (Tanzania Agricultural Development Bank (TADB)) ili iweze kutoa mkopo wenye masharti nafuu kwa mkulima/kikundi. Mteja atachukua Proforma Invoice kutoka NDC na kuwasilisha kwenye TADB. Mteja akikidhi vigezo vya mkopo, utaratibu utafanyika ili kuijulisha NDC kwa bidhaa zitakazokuwa zimeidhinishwa na Benki hii. Baada ya Benki hii kuingiza fedha katika akaunti ya NDC, utaratibu wa kumkabidhi mteja husika bidhaa alizolipia utafanyika.

ii.) Mfuko wa Pembejeo wa Taifa (AGITF)

Utaratibu wa mikopo utafanyika vile vile kwa kupitia Mfuko wa Pembejeo wa Taifa (Agriculture Inputs Trust Fund (AGITF) ) ili uweze kutoa mkopo wenye masharti nafuu kwa mkulima/kikundi. Mteja atachukua Proforma Invoice kutoka NDC na kuwasilisha kwenye mfuko wa Pembejeo. Mteja akikidhi vigezo vya mkopo, utaratibu utafanyika ili kuijulisha NDC kwa bidhaa zitakazokuwa zimeidhinishwa na Mfuko huo. Baada ya Mfuko huo kuingiza fedha katika akaunti ya NDC, utaratibu wa kumkabidhi mteja husika bidhaa alizolipia utafanyika. Shirika linaendelea kuzungumza na Taasisi mbalimbali za fedha ili ziweze kushiriki kutoa mikopo yenye masharti nafuu.

3. Mauzo kwa Mikopo Kupitia kwa Waajiri

i) Kupitia Ofisi ya Bunge

Utaratibu unakamilishwa kuwawezesha Waheshimiwa Wabunge na wafanayakzi katika Ofisi ya Bunge waweze kununua matrekta haya kama mchango wao katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini. Shirika litawakopesha Waheshimiwa Wabunge na Wafanyakazi wa ofisi ya Bunge kwa utaratibu maalum baada ya kutoa malipo ya awali (down payment) siyo chini ya asilimia 40 na kiasi kilichobaki watakopeshwa. Ofisi ya bunge itadhamini mkopo huu kwa wahaeshimiwa Wabunge and Wafabnyakazi wa ofisi hiyo. Aidha, dhamana ya mkopo itakuwa ni msahara na mafao ya mteja husika.

ii) Kupitia Wafanyakazi wa Serikali

Shirika, kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, linakamilisha utaratibu wa kuwawezesha Makatibu Wakuu wa Wizara husika kuwadhamini wafanyakazi wao wanunue matrekta ya aina ya URSUS na zana zake kwa njia ya mkopo. Wafanyakazi wa Serikali watatakiwa kulipa malipo ya awali (down payment) ya siyo chini ya asilimia 40 na kiasi kilichobaki watakopeshwa.

iii) Kupitia Halmashauri za Manispaa/Wilaya

Takriban Halmashauri 16 zimewasilisha maombi yao ya kutaka kununua matrekta ya aina ya URSUS kwa njia ya mkopo. Baada ya kupata mahitaji ya matrekta ya wakulima wake, Halmashauri itakusanya fedha na kulipa katika akaunti ya NDC ambapo NDC itatoa matrekta kulingana na fedha iliyokusanywa. Halimashauri inaweza kununua matrekta haya kwa kupitia benki tajwa haopo juu au kutoa malipo ya awali (down payment) yasiyopungua asilimia 40 na kiasi kinachobakia kitakuwa mkopo wenye masharti nafuu, ikiwemo riba, muda wa kulipa deni na awamu za ulipaji (installments). Ofisi ya Rais – TAMISEMI ndiyo itakuwa mdhamini wa Halmashauri ambazo zitahusika katika mpango huu.

iv) Kupitia Taasisi za Umma

Taasisi za Umma zitaweza kinunua matrekta pamoja na zana zake kwa mkopo ama kwa kupitia Benki iliyotajwa hapo juu au kwa kuwasiliana na NDC ili kuangalia namna bora ya kununua matrekta haya.