Kamati ya Bunge yatembelea TAMCO

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ikiwa imeambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Innocent Bashungwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Ludovick Nduhiye pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Prof. Damian Gabagambi wakitembelea miradi mbalimbali inayopatikana eneo la viwanda la TAMCO, Kibaha, mkoani Pwani

Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imetembelea eneo la viwanda la TAMCO lililopo Kibaha, mkoani Pwani.


Katika ziara hiyo wametembelea na kujionea viwanda mbalimbali vilivyopo katika hatua ya ujenzi kama kiwanda cha GF Trucks kinachotarajiwa kuunganisha magari pamoja na kiwanda cha kuzalisha chanjo za wanyama cha Heister Bioscience Africa Ltd.


Mbali na hapo, kamati hiyo ya bunge ilipata fursa ya kutembelea viwanda vinavyofanya kazi kama kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza mazalia ya mbu cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) pamoja na kiwanda cha kuzalisha vifungashio cha Global Packaging.


kamati hiyo imefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) katika uendelezaji wa eneo hilo na kuwasihi kushugulikia changamoto mbalimbali zinazo jitokeza na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.


Eneo la viwanda la TAMCO lina ukubwa wa hekari 201.63 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya sekta mbalimbali kama dawa, kilimo, nguo na vyombo vya moto.