MIRADI YA LIGANGA, MCHUCHUMA MBIONI KUANZA

Miradi ya Chuma cha Liganga na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma inayomilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), iliyopo Wilayani Ludewa mkoani Njombe kuwa na tija kwa taifa siku za usoni.

Hii ni baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kusema kuwa ni wakati wa kuhakikisha miradi hii inaanza kufanya kazi.

"Kuhusu Mchuchuma na Liganga, nimeshatoa maelekezo. Serikali inaendelea na mazungumzo na wawekezaji kuona tatizo ni nini. Serikali inaweza kujitoa hadi wapi, muwekezaji ajitoe hadi wapi, na kwa sasa duniani chuma kimepanda bei, ni wakati wa kuharakisha mradi ufanye kazi," ameeleza Rais Samia.

Ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Biashara Tanzania, jijini Dar es Salaam.