NDC QUEENS YATINGA NUSU FAINALI

Ligi DAraja la 3 Mkoa

NDC Queens yatinga hatua ya Nusu Fainali, Ligi ya Netball Daraja la 3 Ngazi ya Mkoa baada ya kuzamisha jahazi la timu ya Upendo kwa magoli 26 - 25 kwenye mchezo wa kukata na shoka uliochezwa jijini Dar es Salaam.

NDC Queens iliyo chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), inaingia hatua ya Nusu Fainali bila kupoteza mchezo wowote katika kundi lake.

Mchezo wa kwanza waliwabamiza Tanroads goli 27 - 21, kisha KSN 32 -16, TBS 23 - 15 kabla ya kufunga dimba kwa kuwacharaza Upendo kwa goli 26 - 25.

Leo NDC Queens itashuka dimbani mishale ya saa 9 Alasiri, kuvaana na Tanesco kuwania nafasi ya kusonga hatua ya Robo Fainali.