NDC, TEMDO, CAMARTEC kuleta mapinduzi Sekta ya Kilimo nchini

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa amezindua jembe la kukokotwa na trekta maalum kwa ajili ya kuendeleza sekta ya kilimo hapa nchini, kazi iliyohusisha taasisi 3 zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ya NDC, TEMDO na CAMARTEC.

Zoezi hilo limefanyika tarehe 3.7.2020 ikiwa ni uzinduzi rasmi wa Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara, maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Kilwa Road, Dar es Salaam.

Hatua ya utengenezaji wa jembe na zana nyingine za kilimo ulifadhiliwa na NDC, kutengenezwa na TEMDO kisha kufanyiwa majaribio na CAMARTEC. 

Zana hizo za kilimo zinatarajiwa kuzalishwa na kiwanda cha KMTC kilichopo Hai, mkoani Kilimanjaro ambacho kinasimamiwa na NDC.


Upatikanaji wa zana za kilimo kwa urahisi, utarahisisha ukuaji wa Sekta ya Kilimo nchini na kuchangia pato la taifa na kumuinua mkulima kiuchumi.