NDC, TEMDO KUSHIRIKIANA KUZALISHA MITAMBO

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limeingia makubaliano ya ushrikiano na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo (TEMDO) katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la utafiti , kubadilishana ujuzi pamoja na kuongeza uzalishaji katika kiwanda cha KMTC, cha mkoani Kilimanjaro kinacho milikiwa na NDC.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa makubaliano hayo Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC, Dkt. Nicolaus Shombe amesema  makubaliano hayo yatasaidia kuongeza ufanisi katika uzalishaji pamoja na kupunguza gharama za kuagiza mitambo kutoka nje ya nchi.

Ameongeza kuwa TEMDO wanauwezo wa kuzalisha mitambo sita kwa mwaka hivyo kwa kushirikiana nao wataweza kuzalisha mitandambo mingi na kuuza mpaka nje ya mipaka ya Tanzania. 

"Eneo kubwa kuliko yote ni eneo la utaalamu. Wataalamu wetu wanaweza kwendai TEMDO kujifunza na wao wakaja kwetu  kujifunza vitu mbalmbali" amesema Dkt. Shombe.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa  TEMDO Profesa Fredrick Kahimba amesema matarajio ya mashirikiano katika taasisi hizo mbili ni pamoja na kuongeza ubora wa bidhaa , kupunguza matumizi ya fedha za kigeni na kuzalisha ajira kwa watanzania.

"Kwa kushirikiana na KMTC tutaweza kutengeneza minara ya umeme ambayo tulikuw tunanunu kwa bei ya juu sana nje ya nchi, lakini pia itakapotaka kutengenezwa tutakuwa tunatengeneza hapa hapa kwahiyo tutakuwa tumeisaidia Serikali kwa kiwango kikubwa sana," amesema Professa Kahimba.