NDC yadhamiria kuinua viwanda nchini

NDC kwa kushirikiana na TANCOAL wamemkabidhi Mzee Reuben Mtitu (Mzee Kisangani) tani 60 za makaa ya mawe kwa ajili ya kuendeleza kazi yake ya uhunzi, Ludewa mkoani Njombe. Mzee Mtitu alianza shughuli ya uhunzi miaka 20 iliyopita na anaishukuru Serikali, NDC pamoja na TANCOAL kwa msaada huo kwani utatimiza azima yake ya kuendeleza Tanzania ya viwanda.

Amesema kuwa shughuli hiyo itasaidia kupunguza vitendo ya uharibifu wa miundombinu kwa kuiba vyuma na kusingizia vyuma chakavu kwani vijana wataweza kujiajiri katika shughuli hiyo ya kuyeyusha chuma na kutengeneza zana mbalimbali.Naye Waziri wa Madini, Mh. Dotto Biteko amesema kuwa anatamani siku za usoni akute eneo hilo lina kiwanda kikubwa cha kuyeyusha chuma.

Makabidhiano hayo ya makaa ya mawe kwa Mzee Mtitu yamekuja baada ya maagizo kutoka kwa Waziri wa Madini, Mh. Dotto Biteko (Mb) kuzitaka taasisi za NDC na TANCOAL kumshika mkono Mzee Mtitu ili ajiendeleze zaidi.