
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Nicolaus Herman Shombe kuwa
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Shombe alikuwa Kamishna wa Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango. Dkt. Shombe anachukua nafasi ya marehemu, Prof. Damian Gabagambi.
Uteuzi huo umeanza tarehe 29
Oktoba, 2021.