
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema
Serikali itaendelea kuliwezesha Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa kishirikiana na Taasisi nyingine za Umma katika uzalishaji na usambazaji wa viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi wa mbu waenezao ugonjwa wa malaria.
Dkt. Kijaji ameyasema hayo wakati wa utoaji wa Taarifa ya Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi waenezao ugonjwa wa malaria (Tanzania Biotech Products - TBPL) kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Februari 4, 2022 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Erick Shigongo (Mb) amesema Kamati hiyo imedhamiria kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini na iko tayali kushirikiana na Wizara kuona Shirika hilo linafanya kazi kwa ufanisi katika kuzalisha viuadudu hivyo vinavyoua viluwiluwi wa mbu waenezao ugonjwa wa Malaria na kusambaza nchi nzima ili kuokoa maisha ya watanzania wengi.
Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha uzalishaji na kuweka utaratibu mzuri wa ununuzi na usambazaji wa viuwadudu vianvyouwa viluwiluwi wa mbu waenezao malaria ili kutokomeza malaria nchini.
Akitoa taarifa hiyo ya Kiwanda cha TBPL kwa wajumbe wa kamati hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC). Dkt. Nicholas Shombe amesema Serikali imeanzisha Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi vya mbu waenezao Malaria na magonjwa mengine Dengue, Zika, Chikungunya, Matende na Mabusha ili kutokomeza magojwa hayo nchini.
Kiwanda hiki cha TBPL kilichopo mkoani Pwani, kinamilikiwa na Serikali kwa 100% chini ya NDC na kina uwezo wa kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu, viuatilifu vya kibalojia (bio - pestcides) kwa ajili ya kuua wadudu wadhurifu katika mazao pamba na mbogamboga na mbolea rafiki kwa mazingira (bio - fertilizer).
Kiwanda hiki cha TBPL kilichopo mkoani Pwani, kinamilikiwa na Serikali kwa 100% chini ya NDC na kina uwezo wa kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu, viuatilifu vya kibalojia (bio - pestcides) kwa ajili ya kuua wadudu wadhurifu katika mazao pamba na mbogamboga na mbolea rafiki kwa mazingira (bio - fertilizer).