TAMISEMI WAAMUA KUTOKOMEZA MALARIA

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI) kwa sauti moja wameipokea Kampeni ya Kutokomeza Malaria kwa kutumia viuadudu vinavyo zalishwa na kiwanda cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) kiwanda kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

Kikao hicho kilichokua na lengo la kutambulisha Kampeni Kubwa ya Kitaifa ya Kutokomeza Kabisa mbu na Malaria, ilihusisha Maafisa Kutoka NDC, TBPL pamoja na Kumekucha Tanzania, Asasi isiyo ya Kiserikali iliyopewa jukumu na NDC la kuhamadisha matumizi bora ya viuadudu na kutafuta masoko.

Ushiriki wa OR-TAMISEMI katika kampeni hii ya kitaifa ya kutokomeza Malaria itasaidia kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari za Malaria pamoja na matumizi ya afua zote hasa matumizi sahihi ya viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi vya mbu vinavyo zalishwa na Kiwanda kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) cha TBPL kilichopo Kibaha, Pwani.

Pia, ushiriki huo wa OR-TAMISEMI utasaidia kufikia masoko mapya ambayo yatasaidia kabisa kutokomeza mbu katika makazi yetu na hatimaye kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria.

Semina kwa Wajumbe wa OR-TAMISEMI ilitolewa na Jackson Stephano kutoka Kumekucha Tanzania.

Lengo la NDC kupita kiwanda chake cha TBPL kwa kushirikiana na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Kumekucha Tanzania ni kuhakikisha Malaria inatokomezwa kabisa nchini.

#ndc #Oatamisemi #shirikalataifalamaendeleo #nationaldevelopmentcorporation #tbpl #tanzaniabiotechproductslimited #biolarvicides #endmalaria #saynotomalria