TANZIA

Menejimenti na Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) tunasikitika kutangaza kifo cha Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC, Prof. Damian Gabagambi kilichotokoea siku ya Jumanne, tarehe 20.10.2020 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa Marehemu, Oyster Bay, Dar es Salaam. Menejimenti na Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu.


“BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA. JINA LAKE LIHIMIDIWE”