Tuwekeze katika viwanda vya vifaa tiba nchini kwetu.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. John Jingu alipotembelea jengo la Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) katika viwanja vya Sabasaba na kujionea kazi kubwa inayofanywa na Shirika hasa katika ujezi wa kiwanda kipya cha kuzalisha vifaa tiba cha Afya Technology Manufacturing Company kinacho tarajiwa kujegwa Kibaha mkoani Pwani.
Amesema kuwa NDC pamoja na wadau wengine wanafanya kazi kubwa sana katika kuhakikisha afya za Watanzania na taifa linakua katika hali bora.
Pia amevutiwa na kazi inayofanywa na TANCOAL kwa kukiwezesha kikundi cha wakina mama, Mbalawala Women Group kujikwamua kiuchumi kwa kuzalisha mkaa mbadala kwa kutumia vumbi la makaa ya mawe.