ZABUNI YA KUUZA VIUADUDU

SHIRIKA LA TAIFA LA MAENDELEO

MWALIKO WA KUONESHA NIA YA KUWA WAKALA WA UUZAJI WA VIUADUDU VINAVYOZALISHWA NA KAMPUNI YA TANZANIA BIOTECH PRODUCT LIMITED

UTANGULIZI

Tanzania Biotech Product Limited (TBPL) ni kampuni tanzu ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) inayozalisha viuadudu katika kiwanda chake kilichopo Kibaha, Mkoa wa Pwani. Viuadudu ni bidhaa za kibiolojia ambazo hutumika kuua viluwiluwi wa mbu waenezao ugonjwa wa malaria, dengu na mabusha.

Kiwanda kinazalisha aina mbili za viuadudu ambazo ni “Griselesf” na “Bactivec”. Viuadudu hivi vinatarajia kupunguza kwa kiasi kikubwa na kutokomeza tatizo la ugonjwa wa malaria pamoja na magonjwa mengine yanayoenezwa na mbu hapa nchini. Utokomezaji wa magonjwa haya utasaidia kuwa na jamii/nguvu kazi yenye afya bora kwa ajili ya ujenzi wa Taifa.

Shirika la Taifa la Maendeleo linapenda kuwaalika mawakala wazoefu kuonesha nia ya  kuuza/kusambaza  viuadudu kwa jumla au rejereja kwa niaba ya TBPL.


LENGO

Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa viuadudu vinasambazwa na vinapatikana nchi nzima.


UPATIKANAJI WA MAWAKALA

Shirika litafanya mchujo wa kuwapata  mawakala mahiri katika kila  wilaya watakao   pewa  jukumu la kuuza/kusambaza bidhaa za viuadudu ambazo zipo katika aina na ujazo ufuatao.


Bactivec (Bacillus thuringiensis SH-14 STARAIN 266/2): mililita 30 nadumu la lita 20.

Griselesf (Bacillus sphaericus strain 2362): dumu la lita20.


MAHITAJI

Mawakala ambao wataonesha  nia ya kuuza/kusambaza viuadudu katika sehemu mbalimbali za nchi wanatakiwa kuwasilisha taarifa zifuatazo:


Taarifa za kampuni, ikiwemo jina, mwaka wa kuanzishwa kwake pamoja na maelezo ya mawasiliano (Anwani halisi ya eneo ilipo ofisi ya Kampuni, sanduku la posta, barua pepe, namba ya simu ya mwakilishi wa Kampuni tajwa kwa mawasiliano). Aidha, vivuli vya   vyeti vya usajili kutoka katika mamlaka husika lazima viambatishwe.

Taarifa za kampuni (Company Profile) pamoja na wasifu wa watu muhimu wa Kampuni (CVs).

Mapato ya mwaka ya Kampuni  kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mahitaji ya hapo juu ndio yatakayotumika kama sifa za msingi wakati wa kufanya tathmini.


MASHARTI MUHIMU

Wale watakaokidhi vigezo na masharti ndio watakaojulishwa ili kuwasilisha Andiko la namna ya kutekeleza uwakala wake katika eneo husika.

Katika uwasilishaji wa ombi la nia ya kuwa wakala ni lazima uwasilishe nakala nne (4) (nakala moja halisi pamoja na tatu za vivuli) zikiwa zimewekwa kwenye bahasha iliyofungwa na juu yake imeandikwa “Maombi ya Kuonesha Nia ya Kuuza Viuadudu kwa Niaba ya Tanzania Biotech Product Limited, Kampuni Tanzu ya Shirika la Taifa la Maendeleo.

Mwisho wa kuleta maombi utakuwa  tarehe 7/02/2020 saa 4 kamili asubuhi. Maombi yatafunguliwa maramoja mbele ya wawakilishi wa waombaji, katika ofisi za Shirika la Taifa la Maendeleo, zilizopo mtaa wa Kivukoni Front/ Ohio,ghorofa ya sita, chumba namba 606.

Maombi yoyote yatakayowasilishwa mara baada ya muda uliotajwa kupita hayatapokelewa.

Shirika lina haki ya kuendelea au kukataa zoezi zima la utoaji wa zabuni pasipo kutoa sababu yoyote.

Malalamiko au maswali kuhusiana na utoaji wa zabuni hii lazima yafike kwa maandishi kwa anwani ifuatayo.

Mkurugenzi Mwendeshaji,


Shirika la Taifa la Maendeleo,


P.O Box 2669,


DAR -ES- SALAAM


Tafadhali zingatia kuwa kuonesha nia tu peke yake hakumaanishi kuwa tayari umekwishaingia makubaliano yoyote na NDC.