SISI NI MABINGWA NDANI YA NJE YA UWANJA

"Sisi ni mabingwa ndani na nje ya uwanja." Hii ni kauli ya mchezaji na kapteni wa timu ya mpira wa miguu ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Harrison Jackson wakati wa mahojiano na kituo cha EFM kwenge kipindi cha michezo cha #SportsHQ kuelekea bonanza la michezo la Ocean City linalo tarajiwa kufanyika Jumapili ya tarehe 18.09.2022 viwanja vya TPDC, Jijini Dar es Salaam.

Amezitahadharisha timu shiriki wajiandae kisaikolojia kwani ushindi lazima urudi nyumbani kwani historia ipo wazi kwa timu za michezo za NDC kuwa na ubabe wa kuzifunga timu pinzani kwenye michezo ya mpira wa pete "Netball" pamoja na mpira wa miguu.