MENU

WAZIRI JAFO AIPONGEZA NDC KWA KAZI NZURI

Mradi wa kwanza wa kuzalisha chuma nchini na Afrika Mashariki wa Maganga Matitu unatarajiwa kuanza utekelezaji Januri 2025 na tayari mwekezaji amepatikana huku uwekezaji wake ukifikia dola milioni 77.4.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Nicolaus Shombe alisema hayo Dares Salaam mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara alipotembelea shirika hilo kuzungumza na wafanyakazi.

Alisema mkataba kwa ajili ya kuanza kwa mradi huo utasainiwa ijumaa wiki hii(Agosti 2,2024) na wanatarajia kuanza kuchimba kiasi cha tani milioni moja kwa mwaka lakini kadri uwekezaji unavyoendelea wanaweza kuongeza pia.

Alisema mwekezaji anaaza kulipa fidia watu wapndoke na kuweka mashimo Kwa ajili ya kuanza. “Mkataba wa mradi huu una mpango wa utekelezaji kwamba mwekezaji asipotekeleza mkataba unaweza kusitishwa,” alisema Shombe na kuongeza kuwa katika uwekezaji huo, mwekezaji atakuwa na asilimia 64 na Serikali 36.

Akimtaja mwekezaji huyo kuwa ni Fujian Hexingwang Industry Tanzania Co. Limited ambaye wameingia naye ubia na kwamba yuko nchini na ana kiwanda kingine hapa. Shombe alisema Kwa sasa hivi viwanda vyote vya chuma vinatumia malighafi za chuma chakavu, hivyo kiwanda hicho kitazalisha chuma ghafi ambazo zitatumiwa na viwanda vingine na bidhaa nyingi za chuma zitasaidika na kiwanda hicho.

Alisema ukikamilika utakuwa na faida kubwa, kutoagiza tena bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi, lakini pia Tanzania inaweza kuuza nje ya nchi na kupata fedha za kigeni na kusaidia viwanda kupata malighafi na kuongeza ajira na kusaidia taifa.

Kuhusu mradi wa Liganga na Mchuchuma alisema umefikia hatua ya kuanza utekelezaji, kwa maana kwamba taratibu zote ikiwamo za kufanya tafiti, uchambuzi, upembuzi yakinifu, kupata cheti cha mazingira vinafanyika.

Alisema pia mwaka jana Rais Samia Suluhu Hassan alitoa fedha sh bil 15.4 ambazo zimeenda kulipa fidia kwa waliopo kwenye eneo hilo. Alisema mradi huo ni makubwa wa kuzalisha makaa ya mawe na chuma na hatua zote za maandalizi zimekamilika kuna shughuli zinaendelea kule ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombi ya barabara, na maji.

Shombe alisema mradi mwingine ni wa magadi soda, wa Engaruka ambapo shirika limefanya tafiti zote na hatua iliyobakia kwa sasa ni kutoa fidia ya sh bilioni 14 na uzalishaji uweze kuanza. Akizungumza Jafo aliagiza NDC kuhakikisha miradi yote inafanyiwa kazi na kusimamia taratibu ziweze kukamilika na kupata wawekezaji. Alisema NDC ni shirika kubwa linategemewa na Taifa hivyo liifanye vizuri Kwa kuwa ni roho ya uchumi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *