“Kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu, tutimize wajibu wetu.”
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), wametoa mafunzo ya namna ya kupambana na rushwa mahala pa kazi na nje ya mahala pa kazi kwa wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).
Wafanyakazi wa NDC wamepitishwa kufahamu aina za rushwa, namna ya kutambua aina za rushwa, namna ya kupambana na rushwa na namna ya kuzuia na kuiepuka rushwa. Pia wamepitishwa kwenye sheria na miongozo mbalimbali ambayo itawalinda wasiingie kwenye mitego ya rushwa wanapo tekeleza majukumu yao ndani ya ofisi na nje ya ofisi.