MENU

JAFO AKOSHWA NA SHUGHULI ZA KMTC

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo amefanya ziara ya kikazi Kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine na mitambo mbalimbali cha @kmtctanzania kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kilichopo Mkoani Kilimanjaro.

 

Wafanyakazi wa KMTC wakiendela na shughuli za uzalishaji ndani ya kiwanda cha KMTC

Akiwa kiwandani hapo, Mhe. Jafo amejionea shughuli za uzalishaji wa vipuri na mitambo zinazo endelea, zikiwa zinagusa sekta mbalimbali kama sekta ya madini, nishati, kilimo, uzalishaji na uwekezaji.

Mbali na hayo. Mhe. Jafo ameelezwa pia uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwa kufunga kinu cha kuyeyushia chuma (foundry) pamoja na mtambo wa kutia utandu kwenye chuma (galvanizing plant) ambavyo vimekuwa mkombozi kwenye uzalishaji wa bidhaa za chuma na kusaidia viwanda vingine kunufaika na uwepo wa mitambo hiyo.

#kmtc #ndc #manufacturing #nationaldevelopmentcorporation #shirikalataifalamaendeleo

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *