Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametembelea Mradi wa Kimkakati wa Magadi Soda uliopo Engaruka, mkoani Arusha.
Akiwa ziarani hapo, Waziri Jafo ameelezwa kuwa Magadi ni kemikali inayotumika viwandani kuzalisha vioo, sabuni, rangi, karatasi, kusafishia mafuta ya petroli, kusafishia madini, kutengenezea mbolea na kusafishia
maji. Kwa hiyo, kwa kuvuna magadi hayo, Tanzania itakuwa imeanzisha kiwanda mama na kujiweka katika nafasi nzuri ya kukuza na kuibua kwa kasi viwanda vinavyotumia magadi kama malighafi katika uzalishaji.
Kwa mujibu wa tafiti, Magadi yatakayozalishwa yataweza kutosheleza mahitaji ya magadi hapa nchini na mengine kuuzwa nchi za nje.