Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Dkt. Nicolaus Shombe ameongoza kikao kazi na UNDP Tanzania.
Kikao hiko kimelenga kujadili fursa za ushirikiano kati ya UNDP na NDC katika maeneo mbalimbali ya maendeleo,hasa katika sekta za kilimo, madini na uwekezaji hususan katika maeneo yanayomilikiwa na NDC.
Kwa upande wake Dkt. Shombe alieleza fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatokana NDC pia amesisitiza kuwa NDC ina dhamira ya kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kufanikisha ajenda ya maendeleo ya taifa.
Aidha, Dkt. Shombe ameeleza kuwa anathamini ujio wa UNDP na kushiriki kwake katika jitihada za kukuza uzalishaji na viwanda nchini. Amesisitiza dhamira ya NDC kuwa mkono wa Serikali wa uwekezaji ambapo NDC haitegemei uzoefu mmoja bali itashirikiana na wadau mbalimbali, Serikali, UNDP, sekta binafsi, wakulima, wawekezaji ili kufanikisha miradi ya maendeleo ya taifa.
Kwa upande wa Mwakilishi mkazi wa @undptz (UNDP),Bw. Shigeki Komatsubara ameonesha utayari wa UNDP kushirikiana na NDC, hasa kupitia kampuni tanzu ya NDC, Tanzania Biotech Products Limited (TBPL), katika kutoa msaada kwa wakulima mfano kupitia upatikanaji wa viuatilifu hai kwa makundi ya wakulima ili kuleta mabadiliko chanya katika kilimo.

