NDC YASHIRIKI UZINDUZI WA DAWA YA KUTOKOMEZA KISUKARI

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Dkt. Nicolaus Shombe amezindua dawa ya kupambana na ugonjwa wa kisukari, inayozalishwa na kiwanda cha Labiofam cha nchini Cuba. Hafla hiyo imefanyika wakati wa Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Havana – Cuba yanayofanyika kwa siku 4, kuanzia tarehe 4 mpaka 9 Novemba, 2024.

“Nawapongeza Labiofam kwa hatua hii kubwa,” alisema Dkt. Shombe na kuonesha uwezo wa kiwanda cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) kinacho milikiwa na Serikali kikiwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa mbalimbali za kibaiolojia.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC, Dkt. Nicolaus Shombe (katikati), akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda vya kuongeza Thamani kutoka NDC, Esther Mwaigomole (kulia), na Meneja Uzalishaji wa TBPL, Gasper Kimbi (kushoto) wakiwa kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Havana – Cuba.

Dkt. Shombe alieleza kuwa kiwanda cha TBPL ni cha kipekee barani Afrika, hivyo ni fursa kwa bidhaa hiyo kuzalishwa nchini na kuokoa afya za Watanzania na Waafrika kwa ujumla.

Aliendelea kueleza TBPL inazalisha bidhaa mbili, moja ni ya kupambana ma wadudu dhurifu kwenye mazao na nyingine ni ya kuangamiza viluwiluwi vya mbu waenezao malaria na bado kuna fursa ya kuongeza bidhaa nyingine za kibaiolojia kwa kutumia teknolojia iliyopo kiwandani hapo.

Akiwa nchini Cuba, Dkt. Shombe na ujumbe wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda vya kuongeza Thamani kutoka NDC, Esther Mwaigomole na Meneja Uzalishaji wa TBPL, Gasper Kimbi wamepokelewa na Rais wa kiwanda cha Labiofam, Ndg. Rodi Ortiz ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano baina ya pande hizo mbili kupitia kiwanda cha TBPL.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *