Mapema leo hii 15/10/2025 NDC yapokea ugeni kutoka mfuko wa misitu Tanzania (TaFF ) ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano wa taasisi hizo mbili, ugeni huo ulikuwa na lengo la kufanya tathmini ili kujua changamoto maoni na mapendekezo katika kutekeleza mradi wa kuendeleza shamba la miti ya mpira liliyopo Kalunga mkoani Morogoro
Ushirikiano huo ulikuja baada NDC kupokea ruzuku kiasi cha mil. 402 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kupanda miti ya mpira ambapo mpaka sasa kiasi cha Shilingi milioni201 kimepokelewa na kuweza kupanda miti katika hekta zipatazo 38.5
Naye mkurugenzi wa kuongeza thamani ndugu Esther Mwaigomole amewapongeza TaFF na kuwashauri kuongeza ushirikiano katika maeneo ya utafiti na utunzaji wa miti ya mpira na si upandaji peke yake iliĀ kiuweza kufikia malengo yaliyowekwa.