Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kupitia Kampuni tanzu inayozalisha viuatilifu hai TBPL iliyopo Kibaha mkoani Pwani imepokea ugeni kutoka Labiofam nchini Cuba, waliofanya Ziara kikazi ya siku tatu ikiwa ni pamoja na kutembelea kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za kibiolojia cha TBPL kilichoko Kibaha mkoani Pwani ikiwa ni matunda ya Ziara iliyofanyika Mapema mwezi Februari 2025 na rais wa Bunge la Cuba Bwana Fernandiz Lazzo.
Katika Ziara hii NDC limepata wasaa wa kufanya majadiliano na mwakilishi kutoka kampuni ya Labiofam ya Cuba Bwana Julio Bomet namna nzuri ya kuboresha na kukuza Zaidi kiwanda hiki ikiwa ni pamoja na kujikita katika uzalishaji wa bidhaa nyingi Zaidi za kibiolojia na kuongeza uzalishashaji wa bidhaa kwa kiwango kikubwa Zaidi.
Kwa upande wake Labiofam imekubali kuchangia katika suala zima la Teknolojia itakayochangia ajenda kuu ya Taifa la Tanzania ya kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030.
Aidha Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe amesema ujio wa ugeni huo kutoka Cuba na kutembelea katika kiwandani hicho ni ishara ya kuimarika kwa ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Cuba na tutahakikisha wanashirikiana na Cuba katika kuhakikisha kiwanda hicho kinazalisha idhaa mbalimbali za kibaolojia.
Kwa upande wa Bwana Julio Gomez ameanisha kuwa Cuba iko tayari kuchangia katika swala zima la kuangamiza Malaria kupitia uzalishaji mkubwa kwa bidhaa za kutokomeza Malaria ikiwa ni ishara ya ushirikiano mzuri baina ya Cuba na Tanzania
Tanzania na Cuba zina ushirikiano mkubwa katika sekta mbalimbali ambao ulioasisisiwa na hayati baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere pamoja na rais wa Cuba Fidel Castro.