Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo mapema hii leo amefanya ziara ya kikazi katika bandari kavu ya ETC Cargo ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ambayo inapatikana Mbagala jijini Dar es Salaam.
Katika Ziara hiyo Mh. Jafo alipata wasaa wa kukagua shughuli mbalimbali za utendaji zinazofanywa na kampuni hio.
Aidha Waziri Jafo alipata wasaa wa kuzungumza na watendaji wa bandari hiyo pamoja na watumishi wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), amepongeza ushirikiano mzuri uliopo baina ya NDC na ETC Cargo kwa juhudi wanazozifanya ikiwa ni pamoja ongezeko la ajira zaidi 139 za kudumu na 600 zisizo zakudumu.
Waziri Jafo pia ametoa siku arobaini na tano za majadiliano kati ya ETC Cargo na NDC ili kuweka mikakati bora zaidi kwa maslahi mapana ya Taifa.