MRADI WA CHUMA WA MAGANGA MATITU KUTEKELEZWA HIVI KARIBUNI KWA USHIRIKIANO WA SERIKALI NA MWEKEZAJI
Serikali imeeleza dhamira yake ya kuanza utekelezaji wa Mradi wa Chuma wa Maganga Matitu kwa haraka, kwa kushirikiana na mwekezaji wa kimataifa, ili kuhakikisha rasilimali hiyo muhimu inatumika kwa manufaa ya taifa. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo, alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo […]