Habari

NDC YASHIRIKI UZINDUZI WA DAWA YA KUTOKOMEZA KISUKARI

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Dkt. Nicolaus Shombe amezindua dawa ya kupambana na ugonjwa wa kisukari, inayozalishwa na kiwanda cha Labiofam cha nchini Cuba. Hafla hiyo imefanyika wakati wa Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Havana – Cuba yanayofanyika kwa siku 4, kuanzia tarehe 4 mpaka 9 Novemba, 2024.

NDC YASHIRIKI UZINDUZI WA DAWA YA KUTOKOMEZA KISUKARI Read More »

NDC YAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA KOREA KUWEKEZA KATIKA MIRADI YAKE

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limewaalika wawekezaji kutoka Korea kuwekeza katika miradi ya kimkakati inayosimamiwa na shirika hilo, hatua inayolenga kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda nchini. Hayo yameelezwa leo katika semina ilichofanyika katika hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, iliyojumuisha NDC,

NDC YAWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA KOREA KUWEKEZA KATIKA MIRADI YAKE Read More »

JAFO ZIARANI MRADI WA MAGADI SODA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametembelea Mradi wa Kimkakati wa Magadi Soda uliopo Engaruka, mkoani Arusha. Akiwa ziarani hapo, Waziri Jafo ameelezwa kuwa Magadi ni kemikali inayotumika viwandani kuzalisha vioo, sabuni, rangi, karatasi, kusafishia mafuta ya petroli, kusafishia madini, kutengenezea mbolea na kusafishia maji. Kwa hiyo, kwa kuvuna magadi hayo, Tanzania

JAFO ZIARANI MRADI WA MAGADI SODA Read More »

NDC YAVUTIA UWEKEZAJI WA DOLA MILIONI 77.45 KATIKA MRADI WA CHUMA WA MAGANGA MATITU

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limeandika historia mpya kwa kusaini mkataba wa uwekezaji na kampuni ya Fujian Hexingwang, ambao unahusisha uchimbaji wa madini ya chuma. Uwekezaji huu wa kwanza wa aina yake unatarajiwa kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wakazi wa Ludewa, mkoa wa Njombe, na kwa Taifa kwa ujumla. Mkataba huu umesainiwa mjini

NDC YAVUTIA UWEKEZAJI WA DOLA MILIONI 77.45 KATIKA MRADI WA CHUMA WA MAGANGA MATITU Read More »

WAZIRI JAFO AIPONGEZA NDC KWA KAZI NZURI

Mradi wa kwanza wa kuzalisha chuma nchini na Afrika Mashariki wa Maganga Matitu unatarajiwa kuanza utekelezaji Januri 2025 na tayari mwekezaji amepatikana huku uwekezaji wake ukifikia dola milioni 77.4. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Nicolaus Shombe alisema hayo Dares Salaam mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara alipotembelea shirika hilo kuzungumza

WAZIRI JAFO AIPONGEZA NDC KWA KAZI NZURI Read More »

WAZIRI JAFO AZITAKA HALMASHAURI NCHINI KUTOKOMEZA MALARIA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo amezitaka halmashauri zote nchini kununua viuadudu vya kuangamiza mazalia ya mbu ili kuondokana na ugonjwa wa malaria nchini. Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi kiwanda cha kuzalisha bidhaa za kibaiolojia cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL), kilichopo Kibaha mkoani Pwani. Ameeleza kuwa

WAZIRI JAFO AZITAKA HALMASHAURI NCHINI KUTOKOMEZA MALARIA Read More »

NDC KUISAIDIA UGANDA KUANGAMIZA MAZALIA YA MBU

Ujumbe kutoka Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda vya Kuongeza Thamani (DSV), Esther Mwaigomole umefanya mazungumzo ya kibiashara na Mwakilishi wa Balozi wa Uganda, Mwambata Jeshi, Brigedia. Ronald Bigirwa, mazungumzo yaliyolenga kuuza bidhaa za kibaiolojia za kuangamiza mazalia ya mbu na za kuangamiza wadudu dhurifu kwenye mazao. Kikao kilichofanyika

NDC KUISAIDIA UGANDA KUANGAMIZA MAZALIA YA MBU Read More »