Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Dkt. Nicolaus Shombe amefanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknlojia Vijijini, (CAMARTEC), Mha. Pythias Ntela, kikao kilicho dhamiria kuongeza uzalishaji wa vipuri vya mashine pamoja na vyombo vya moto kupitia kiwanda cha KMTC kiwanda kilichopo mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Dkt. Nicolaus Shombe akiwa juu ya trekta linalo zalishwa na TEMDO.
Kikao hicho kilicho wakutanisha Wakurugenzi hao wanaosimamia uendelezaji wa viwanda nchini kimefanyika Makao Makuu ya TEMDO, mkoani Arusha na kupanga mipango mbalimbali ya kuendeleza ushirikiano wa uzalishaji wa mashine na mitambo mbalimbali.
Ikumbukwe mwaka 2018 hadi 2020, NDC na TEMDO walishirikiana kwenye uzalishaji wa zana za kilimo hasa tela zilizo tumika kwenye kilimo hivyo kuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima.
Tela la mizigo linalo zalishwa na KMTC ambalo usanifu wake umefanywa na TEMDO.
Ushirikiano huu wa taasisi hizi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ni ishara njema kwa maendeleo ya Sekta ya Viwanda nchini, kwani utapunguza utegemezi wa taasisi kutoka nje ya nchi hivyo kuwainua uzalishaji wa ndani.