NDC HATUNA MSONGO WA MAWAZO

Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji, Dkt. Nicolaus Shombe wamepata elimu ya kupambana na msongo wa mawazo kutoka kwa mkufunzi Gervas Kolola.

Mafunzo hayo yameangazia aina za msongo, visababishi vya msongo pamoja na kukabiliana na msongo mahala pa kazi na nyumbani.

Pamoja na mambo mengine, wafanyakazi wa NDC wamejifunza mbinu za kuboresha mahala pa kazi kwa kufanya kazi kwa ushirikiano, kwa wakati na kwa usahihi ili kuzuia msongo wa mawazo unaoweza kutokana na mlundikano wa shughuli.