NYIKA AIBUKA MFANYAKAZI BORA NDC 2023

Ili kuongeza ufanisi wa kazi na kuongeza chachu ya utendaji, Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limekua likitambua mchango wa wafanyakazi waliofanya vizuri kwenye shughuli za kila siku za Shirika ambapo zoezi hilo uhusisha ushindani kuanzia ngaziĀ  ya idara na hatimaye kupata Mfanyakazi Bora wa mwaka.

Kwa mwaka 2023, Ndugu Mseli Nyika ameibuka kidedea kama Mfanyakazi Bora wa NDC aliyechaguliwa kwa kishindo na wafanyakazi wenzake, kinyanganyiro kilichofanyika kuelekea kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama MeiMosi.

Katika kinyanganyiro hicho kilihusisha wafanyakazi kutoka idara mbalimbali ndani ya NDC, ambapo kutoka Idara ya Viwanda Mama iliwakilishwa na Kevin Barugahare, Idara ya Viwanda vya Kuongeza Thamani iliwakilishwa na Bi. Hawa Bilia, Idara ya Fedha iliwakilishwa na Hamida Shabani, huku Ofisi ya Mtendaji Mkuu iliwakilishwa na Nelson Mapamba na Mseli Nyika kutoka Idara ya Utawala.

Kutoka kushoto: Israel Mfungo, Hawa Bilia, Hamida Shabani, Dkt. Nicolaus Shombe, Mseli Nyika, Rebecca Masalu na Nelson Mapamba

Akiongea baada ya kukabidhi tuzo hizo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC, Dkt. Nicolaus Shombe aliwapongeza washiriki wote na kuwaeleza wao wote ni washindi kwani wote wana jukumu la kuhakikisha wanasogeza mbele gurudumu la maendeleo kwa manufaa ya Shirika na Nchi kwa ujumla.

Pia aliwasihi wafanyakazi wengine kufanya kazi kwa bidhii bila kusukumwa kwani kwa kufanya hivyo ni kutambua wajibu wao na kutambua dhumuni linalo wafanya waamke kila siku kuja kazini.

Nae, Mseli Nyika aliwashukuru wafanyakazi wenzake wa NDC na kusema bila wao yeye si kitu kwani wote wanategemeana kwenye majukumu yao ya kila siku. Aliendelea kusema wao ni kama timu ya mpira, kila mchezaji ana nafasi yake uwanjani kuhakikisha timu inapata ushindi na Mkurugenzi Mwendeshaji ndiye kocha wao.

Utaratibu wa kutambua Mfanyakazi Bora wa Shirika ulianzishwa mwaka mmoja uliopita na huu ni mwaka wa pili mfululizo tuzo hiyo inakwenda Idara ya Utawala ambapo mwaka uliopita tuzo hiyo ilikwenda kwa swahiba wa Nyika, nduguAlphonce Lufunda.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *