Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amekitaka kiwanda Cha Viuatilifu vya kuua mazalia ya Mbu (TBPL) kilichopo Kibaha Mkoani Pwani kuzalisha bidhaa za Viuatilifu hai kwa ajili ya Msimu huu wa Kilimo kuanzia mwezi Oktoba Mwaka huu.
Dkt. Kijaji ametoa maelekezo hayo Septemba 21, 2023 wakati akizungumza na Uongozi, Watumishi na Waandishi wa habari baada ya kufanya ziara kiwandani hapo kwa ajili ya kuona utekelezaji wa maagizo ambayo aliyatoa kwa ajili ya uboreshaji wa kiwanda hicho hivi karibuni.
Tarehe tarehe 21/6/2023 mamlaka ya udhibiti wa Mimea ilitupatia usajili wa bidhaa hii, hivyo tunaweza kuanza kuzalisha kwa kwa wingi ili kuweza kuwasaidia watanzania kupata mbolea nzuri ambayo haina kemikali pia haiharibu mazingira,na kwenda sambamba na mpango wa mradi wa Kilimo wa BBT amesema Dkt. Kijaji
Nakuongeza kuwa ningependa bidhaa hii Mwezi wa 10 Mwaka huu ianze kuzalishwa kwa wingi na iingie sokoni kwani huu ni msimu wa Kilimo,.
Dkt Kijaji amefafanua kuwa dawa hiyo ni rafiki kwa Mazingira, afya ya Binadamu na mimea. Ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Shirika la Maendeleo la Taifa NDC kwa kutekeleza maagizo aliyotoa alipotembelea kiwanda hicho.
Amesema kuwa dawa ya viluwiluwi vya kuua Mbu inayozalishwa na kiwanda imekubaliwa barani Afrika ambapo hadi sasa imefikia Nchi saba ambazo zinatumia dawa hiyo,miongoni mwake ni Kenya, Angola, Botswana, Msumbiji,Swatin, Niger na hivi karibuni itaanza kupelekwa nchini Uganda.
Hata hivyo ameagiza uongoza kuendelea kutafuta masoko ya bidhaa za kiwanda hicho ndani na nje, pamoja na kuboresha kitengo cha masoko. Kwa pande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe ameeleza kuwa kiwanda hicho kinazalisha bidhaa za kibaolojia za kuulia viluwiluwi vya Mbu pamoja na Bidhaa za Mbolea ya Kilimo.
Amesema kuwa kiwanda hicho ni cha kipekee na cha Kimataifa nakwamba pamoja na kuazalisha dawa hiyo ya viluwiluwi wa mbu lakini pia ni maabara kubwa ya bidhaa za kibaolojia.