MENU

MATUMAINI MAKUBWA KWA BODI MPYA YA TBPL

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na biashara Dkt. Hashil Abdallah amezindua rasmi bodi mpya ya wakurugenzi ya kiwanda cha kuzalisha dawa za kibaiolojia, Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) kilichopo Kibaha mkoani Pwani huku akiitaka bodi hiyo kuhakikisha inachapa kazi katika kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza Sekta ya Viwanda hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo,Katibu Mkuu Dkt. Abdallah amesema kuwa kiwanda cha TBPL ni cha pekee na cha kimkakati na ni dhamira njema ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kinaboresha afya za Watanzania katika kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa Malaria, Chikungunya pamoja na Dengue hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdalla akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya TBPL.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu amewataka wajumbe wapya wa bodi ya TBPL kuhakikisha wanachapa kazi huku akiishukuru bodi iliyomaliza muda wake kutokana na kile walichokifanya katika muda wao wa uongozi na kwamba hawajaondoka kiwandani kwa kuwa busara zao na michango yao bado zinahitajika katika uendeshaji wa kiwanda.

“Kwa kipekee kabisa niwashukuru sana Wajumbe wa Bodi inayomaliza muda wake leo chini ya Prof. Madundo Mtambo kutokana na kile walichokifanya na mnaondoka kwa sababu tu ya utaratibu uliopo na kwamba busara zenu na mchango wanu bado zinahitajika,” alibainisha Dkt. Abdallah.

Mwenyekiti wa Bodi ya TBPL iliyomaliza muda wake, Prof. Madundo Mtambo akiwashukuru Wajumbe wa Bodi iliyopita, Wafanyakazi wa TBPL kwa ushirikiano wako na kuikaribisha bodi mpya ya Wakurugenzi.

Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Bi. Rhobi Sattima licha ya kumshukuru mgeni rasmi kwa ujio wake katika uzinduzi wa bodi hiyo amesema kwa hivi sasa kiwanda cha TBPL kipo katika hatua za mwisho za uzalishaji wa bidhaa mpya ya viuatilifu ambavyo vitakuwa vinatumika kupambana na wadudu dhurifu wa mazao ambapo tayari viuatilifu hivyo vimekwisha pata usajili kutoka katika Taasisi mbalimbali za usajili wa viuatilifu hapa nchini.

Tunakushukuru sana Mgeni Rasmi kwa ushirikiano ambao muda wote mmekuwa mkitupa, naomba nikutaarifu kuwa tayari kiwanda kimefanikiwa kufanya majaribio ya viuatilifu ambavyo vimeonyesha mafanikio makubwa katika kupambana na wadudu dhurifu na hivi ninavyozungumza tayari vimeshapata usajili na vitakuwa vinazalishwa hapa kwa kutumia mitambo hii tuliyonayo” alibainisha Bi. Sattima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi aliyemaliza muda wake Prof. Madundo Mtambo akizungumza kwa niaba ya wajumbe ameshukuru kwa ushirikiano ambao wamepewa katika kipindi chote cha uongozi wao na wanaamini bodi mpya itabadilisha changamoto walizokutana nazo na kuwa fursa.

Kiwanda cha TBPL ni kiwanda pekee barani Afrika na kinamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 ambacho kinatumia teknolojia ya kipekee katika kuangamiza mazalia ya mbu hapa nchini ni matokeo baina ya ushirikiano wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Cuba na kina uwezo wa kuzalisha lita milioni sita kwa mwaka ambazo hutumika katika kupambana na magonjwa yatokananyo na mbu ikiwemo Malaria,Dengue pamoja na Chikungunya.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na biashara Dkt. Hashil Abdallah amezindua rasmi bodi mpya ya wakurugenzi ya kiwanda cha kuzalisha dawa za kibaiolojia, Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) kilichopo Kibaha mkoani Pwani huku akiitaka bodi hiyo kuhakikisha inachapa kazi katika kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza Sekta ya Viwanda hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo,Katibu Mkuu Dkt. Abdallah amesema kuwa kiwanda cha TBPL ni cha pekee na cha kimkakati na ni dhamira njema ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kinaboresha afya za Watanzania katika kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa Malaria, Chikungunya pamoja na Dengue hapa nchini.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu amewataka wajumbe wapya wa bodi ya TBPL kuhakikisha wanachapa kazi huku akiishukuru bodi iliyomaliza muda wake kutokana na kile walichokifanya katika muda wao wa uongozi na kwamba hawajaondoka kiwandani kwa kuwa busara zao na michango yao bado zinahitajika katika uendeshaji wa kiwanda.

“Kwa kipekee kabisa niwashukuru sana Wajumbe wa Bodi inayomaliza muda wake leo chini ya Prof. Madundo Mtambo kutokana na kile walichokifanya na mnaondoka kwa sababu tu ya utaratibu uliopo na kwamba busara zenu na mchango wanu bado zinahitajika,” alibainisha Dkt. Abdallah

Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Bi. Rhobi Sattima licha ya kumshukuru mgeni rasmi kwa ujio wake katika uzinduzi wa bodi hiyo amesema kwa hivi sasa kiwanda cha TBPL kipo katika hatua za mwisho za uzalishaji wa bidhaa mpya ya viuatilifu ambavyo vitakuwa vinatumika kupambana na wadudu dhurifu wa mazao ambapo tayari viuatilifu hivyo vimekwisha pata usajili kutoka katika Taasisi mbalimbali za usajili wa viuatilifu hapa nchini.

Tunakushukuru sana Mgeni Rasmi kwa ushirikiano ambao muda wote mmekuwa mkitupa, naomba nikutaarifu kuwa tayari kiwanda kimefanikiwa kufanya majaribio ya viuatilifu ambavyo vimeonyesha mafanikio makubwa katika kupambana na wadudu dhurifu na hivi ninavyozungumza tayari vimeshapata usajili na vitakuwa vinazalishwa hapa kwa kutumia mitambo hii tuliyonayo” alibainisha Bi. Sattima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi aliyemaliza muda wake Prof. Madundo Mtambo akizungumza kwa niaba ya wajumbe ameshukuru kwa ushirikiano ambao wamepewa katika kipindi chote cha uongozi wao na wanaamini bodi mpya itabadilisha changamoto walizokutana nazo na kuwa fursa.

Kiwanda cha TBPL ni kiwanda pekee barani Afrika na kinamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 ambacho kinatumia teknolojia ya kipekee katika kuangamiza mazalia ya mbu hapa nchini ni matokeo baina ya ushirikiano wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Cuba na kina uwezo wa kuzalisha lita milioni sita kwa mwaka ambazo hutumika katika kupambana na magonjwa yatokananyo na mbu ikiwemo Malaria,Dengue pamoja na Chikungunya.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *