TIA Yatembelea NDC, Yavutiwa na Maeneo ya Uwekezaji

Uongozi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) umetembelea Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa lengo la kuimarisha na kudumisha uhusiano wa kimkakati kati ya taasisi hizo mbili, pamoja na kujifunza fursa za uwekezaji zinazopatikana kupitia maeneo yanayomilikiwa na NDC.

Katika ziara hiyo, ujumbe wa TIA uliongozwa na Prof. Hassanal Issaya na kupokelewa na meneja wa uwekezaji wa NDC, Bwana Revocatus Rashel.

Katika mazungumzo hayo, Bw.Rashel aliwasilisha na kueleza miradi mbalimbali ya uwekezaji inayosimamiwa na Shirika, ikiwemo fursa zinazopatikana katika maeneo ya uwekezaji yanayomilikiwa na NDC.

Nao uongozi wa TIA ulipata fursa ya kufahamu zaidi kuhusu maeneo hayo na fursa zilizopo, ikiwemo uwezekano wa kutumia baadhi ya maeneo hayo kwa ajili ya shughuli za elimu. TIA ilieleza kuvutiwa na fursa hizo na kuonesha nia ya kuangalia uwezekano wa kuanzisha chuo katika moja ya maeneo ya uwekezaji yanayomilikiwa na NDC.

NDC imesisitiza umuhimu wa ushirikiano na taasisi mbalimbali katika kuchochea matumizi yenye tija ya maeneo ya uwekezaji na kuongeza fursa za maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Ziara hiyo pia imekuwa fursa ya kuendelea kujenga mahusiano yatakayowezesha taasisi hizo kushirikiana katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *