MENU

RAIS WA LABIOFAM YA CUBA KIWANDANI TBPL

Kiwanda pekee barani Afrika cha kuzalisha viuadudu vya kuangamiza mazalia ya mbu, Tanzania Biotech Products Limited (TBPL), kimetembelewa na Rais wa Labiofam kutoka Cuba, Rodi Valdes Ortiz ikiwa ni ziara ya kujionea utendaji kazi wa kiwanda hicho kilichopo Kibaha, mkoani Pwani.

Akiwa kiwandani hapo amefanya mazungumzo na Menejimenti ya TBPL pamoja na watendaji wa NDC wakiongozwa na Dkt. Yohana Mtoni na Esther Mwaigomole, ambapo amewapongeza watendaji hao na wafanyakazi wa kiwanda hicho kwa kazi wanayoifanya na kuwataka waongeze kasi ya kuzalisha viuadudu pamoja na viuatilifu kwani uhitaji wa soko ni mkubwa sana.

Mbali na uzalishaji wa viuadudu, kiwanda hicho pia kimeanza kuzalisha viuatilifu kwa ajili ya kuangamiza wadudu dhurifu kwenye mazao hasa pamba, mahindi nambogamboga, huku ikionesha matokeo mazuri kwenye kuangamiza viwavi kwenye korosho.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *